UTANGULIZI:
(Ubebaji wa maji/mizigo usio sahihi) |
(Upishi usiozingatia afya ya mgongo) |
Ni shughuli
gani zinazochangia kusababisha maumivu ya mgongo?
Shughuli zote
za kila siku zina mchango mkubwa katika kusababisha maumivu ya mongo. Baadhi ya
zilizo bayana ni pamoja na: Kufua, Kudeki, Kupika, Kuosha vyombo, Kufagia
uwanja/nyumba, Kubeba maji/mizigo midogo dogo.
Zinachangiaje
katika kuleta maumivu ya mgongo?
(Athari za kuinma katika diski) |
(Kufua kwa kuinma) |
- Misuli kuvutika sana kupita kiasi na hivyo kuchanika kwa ndani hali mbayo husababisha uvujaji wa damu katika mishipa midogo dogo na kusababisha kuhisi maumivu katika misuli husika. Kafanya kazi katika mkao huo huo kwa muda mrefu au mara kwa mara husababisha mamivu ya muda mrefu.
- Mgandamizo katika pingili za mgongo pamoja na diski zake hali ambayo husababisha kulemewa kwa mgongo kuhimili uzito wa kiwili wili cha juu pamoja na kichwa wakati wa kufanya kazi. Hii hupelekea msuli kujikaza zaidi na hata kupasuka na diski kusogea mbali na mahali pake pa asili hivyo kusababisha maumivu ya mgongo.
(Kufagia kwa kuinama) |
- Kujizuia kuinama
(kabisa au kwa muda mrefu) wakati wa kufanya
shughuli za nyumbani. - Kujua namna ya kujali afya ya mgongo wako wakati wa kufanya kazi ya aina yoyote [angalia mkao mzuri (ni upi?)]
- Kufanya mazoezi hasa ya mgongo kila siku unapoamka na kabla ya kuuingia kulala.
- Kubadilisha au kuboresha namna ya kufanya kazi hizo na/au mazingira ya kufanyia kazi.
(Namna nzuri ya kupika) |
(Dekio la mpini mrefu) |
Kudeki: watu wengi leo hudeki wakiwa wameinama hali ambayo
huwa si rafiki kwa afya ya mgongo. Badala yake wanapaswa kununua au kutumia
dekio lenye mpini mrefu badala ya tambala ambalo huwafanya wainame wakati wa
kufanya kazi hiyo.
Kupika: kama iliyo katika kufua, vile vile jiko nalo linapaswa
kuwa katika urefu sawia ili kupunguza kuinama wakati wa kufua. Unashauriwa kununua
jiko lefu (la umeme, gesi au mkaa) ambalo utapika ukiwa umesimama [kwa wenye
uwezo] au kuweka jiko ulilonalo juu ya meza sawia na urefu wako.
(Mpini wa ufagio uwe mrefu) |
Kuosha vyombo: pa kuoshea vyombo pawe katika urefu stahili
kama livyo katika kufua.
Kubeba maji/mizigo midogo midogo ya nyumbani: zingatia namna
ya ubebaji sahihi wa mizigo ili kupunguza mgandamizo mkubwa katika mgongo wako
[angalia namna sahihi ya kubeba mizigo]
(Ni vyema ukafua ukiwa umesimama) |
***Zingatia***
(Ni bora ukakaa kuliko kuinama) |
Unapofanya kazi ya muda mrefu au ya kurudia rudia mara kwa
mara jaribu kutafuta namna ya kuifanya ukiwa umesimama.
Kama unakaa wakati wa kufanya kazi hakikisha upo katika mkao
mzuri na pia kiti kiwe rafiki kwa kazi husika.
***(Kwa swali au ushauri, usisite kuwasiliana nami)***
No comments:
Post a Comment