UTANGULIZI
(Muhimu kupasha mwili) |
Jamii ya leo hasa vijana wana mwitikio mzuri wa
kufanya mzoezi kwa kutumia vifaa vya kisasa katika “Gym” mbali mbali. Wachache wao
katika kundi hilo la walio wengi katika kushiriki katika mazoezi mbali mbali
hujikuta katika dimbwi kubwa la kupatwa na mtatizo ya kuchanika au kujeruhiwa
kwa misuli hivyo kuonekana kuwa na
maumivu katika misuli yao hasa ya miguu (paja), mikono (bega) na hata ya mgongo
pia.
Changamoto ni kwamba; Je, wanaofaya mazoezi huwa
wanaundaa mwili katika kuyapokea kabla ya kuanza mazoezi husika? Je, unafahamu
umuimu wa kuuandaa mwili kabla ya kuanza mazoezi husika? Na, je, unafahamu
madhara ya kuanza mazoezi bila ya kuuandaa mwili wako katika kuyapokea?
Swali:
Je, ni lazima mwili uandaliwe kabla ya kuanza mazoezi rasmi? Jibu:
kabla ya kuanza mazoezi husika (mazoezi uliokusudia kufanya) ni lazima
uuandae mwili katika kuyapokea kabla ya kuanza kufanya!
(Mazoezi ya viungo) |
Swali:
Je, ni namna gani napaswa kuuandaa mwili kabla ya kuanza mazoezi husika? Jibu:
mwili unaandaliwa kwa kuanza kufanya mazoezi madogo madogo kabla ya
mazoezi rasmi. Mazoezi haya yamegawanywa katika makundi mkuu mwili:
- Ya kunyoosha na kulainisha misuli (pamoja na viungo) --- “Stretching exercises”
- Ya kupasha mwili (misuli na viungo vingine vya mwili) --- “Warm up”
Umuhimu
wa mazoezi haya ya mandalizi:
- Kunyoosha na kurefusha misuli mifupi mwilini
(Andaa moyo wako kwanza) - Kuandaa misuli katika kupokea damu ya kutosha kujiandaa na mazoezi
- Kupunguza hatari ya kuchanika kwa msuli itakayohusika katika mazoezi
- Kuandaa moyo katika kusukuma damu itakayokidhi mahitaji ya mwili wakati wa mazoezi
- Kuandaa mapafu katika kuongeza kasi ya kupokea hewa (Oxygen) ili kupata nishati muhimu wakati wa mazoezi
- Kuongeza mzunguko na ujazo wa damu katika viungo vyote muhimu kabla ya kuanza mazoezi
- Kuandaa mwili kwa ujumla ikiwa ni kiakili pamoja na kimwili katika kuwa tayari kuanza mazoezi
Madhara
ya kutoandaa mwili kabla ya kuanza mazoezi:
- Kupatwa na maumivu ya misuli saa chache au kesho yake baada ya kufanya mzoezi
- Kukosa pumzi ya kutosha kuendelea na mazoezi
- Kuhisi kizunguzungu na hata kuzimia katikati au mwishoni mwa mazoezi
- Misuli kuchanika (hasa ya paja)
- Kuteguka ukiwa mazoezini
- Shinikizo la damu kwa wale wenye matatizo ya moyo au kisukari
“Target”
ya mzoezi haya ya mandalizi:
Mazoezi haya ya kuandaa mwili kabla ya mazoezi rasmi
yanalenga hasa viungo vyote muhimu katika mazoezi kama vile:
(Andaa misuli yako) |
- Misuli
- Moyo
- Mishipa ya damu
- Mapafu
- Maungio (joints)
- Ubongo (damu ya kutosha na kisaikolojia)
***Mazoezi haya ya namna ya kuandaa mwili kabla ya
kuanza mazoezi rasmi yatakujia hivi karibuni***
Yataletwa lini
ReplyDelete