UTANGULIZI
(Unyenyuaji sahihi wa mzigo ) |
Mzigo
unaweza kuwa kitu chochote ambacho kinahitaji nguvu yako binafsi au mashine
katika kukibeba au kukihamisha kutoka eneo moja kwenda jingine. Mzigo unaweza
kuwa mwepesi (wenye uzito wa kuanzia “gramu” katika kipimio cha uzito) au mzito
(“kilogramu” hadi kufikia “tani”).
Katika kipengele
hiki tutalenga katika mizigo ya kubebeka kwa mikono(nguvu) ya binadamu katika
shughuli za kawaida za kila siku; majumbani (kuanzia kilo 5-20), viwandani na maeneo
mengine ya kazi (hadi kufikia kilo 100) na katika michezo/mazoezi (zaidi ya
kilo 100).
Ubebaji/uhamishaji
wa mizigo:
- Mara nyingi
watu hujikuta wakibeba mizigo mizito (kuanzia kilo 5) bila kuzingatia usalama
(Ubebaji usizingatia afya wa mgongo; picha ya 1) - Ubebaji huo usiozingatia usalama na afya ya mgongo ni ule ambao watu hutumia msuli ya mgongo badala ya ile ya miguu katika kubebea mizigo. Mfano, mtu kuinama wakati wa kubeba au kunyenyua mzigo ulio chini zaidi badala ya kuchuchumaa na hivyo kujikuta akitumia misuli ya mgongo (kwa kuinua kiwili wili ikiwa ni pamoja na mzigo) badala ya ile ya miguu (inayopaswa kutumika wakati wa kuinuka).
Madhara ya
kutumia misuli ya mgongo katika kunyenyua/kubeba mizigo:
- Kuweka uzito mkubwa katika mifupa (pingili za uti wa mgongo) ya mgongo wakati wa kunyenyua mzigo.
- Kuongeza mgandamizo katika disk zinazotenganisha pingili za uti wa mgongo hivyo kuzifanya zihame au kugandamiza na pingili za uti wa mgongo kwa mwelekeo wa kukinzana kunakosababisha zipasuke au kuwa na nyufa…
- Kunvunjika kwa pingili za uti wa mgongo hasa kwa wazee (zaidi ya miaka 60)
Matatizo yanayotokana
na ubebaji usiozingatia usalama na afya ya mgongo:
- Maumivu ya mgongo [wa chini (kati ya mbavu na kiuno)na/au wa juu (kati ya mbavu na shingo]
- Maumivu ya kiuno
- Maumivu ya shingo
- Maumivu ya viungo vingine vinavyotegemeana wakati wa ubebaji wa mizigo kama vile: mabega, nyonga, magoti n.k
Ubebaji/unyenyuaji sahihi wa mzigo:
Ili kubeba/kunyenyua
au kuhamisha mzigo kutoka eneo moja hadi jingine kwa kuzingatia usalama wa mgongo wako unapaswa kuzingatia
hatua zifuatazo:
(Hatua za ubebaji wa mzigo) |
- Kabla ya kubeba mzigo kwanza fikiri (panga kwanza) utabeba kutoka wapi hadi wapi. Hakikisha njia utakayopita haina vizuizi (safisha njia/ondoa vizuizi njiani kabla ya kubeba mzigo).
- Hakikisha upo katika mkao wa kukufanya uwe katika stamina ya kuubeba mzigo (mguu pande ili kuuweka mzigo usawa wa katikati ya miguu). [Wanawake wanashauriwa wavae mavazi ambayo yatawaruhusu kukaa mguu pande au kuchuchumaa – mfano; gauni lefu na pana, sketi ndefu na pana au suruali badala ya sketi/gauni fupi na ya kubana]
- Chuchumaa huku mgongo wako ukiwa katika u-wima (sawa na ukiwa umesimama au umekaa katika mkao mzuri) na si kuinama wkati wa kubeba mzigo.
- Hakikisha umeshika mishikio ya mzigo au umepata pahali pa kushika mzigo wako vizuri. Hii itapunguza madhara yanayoweza kutokana na kuteleza kwa mzigo uliobeba.
- Beba/nyenyua
mzigo ukiwa karibu na mwili wako hii itakufanya kuwa katika stamina ya kuubeba.
Pia hii inapunguza matumizi ya nguvu nyingi hasa katika kuhusisha misuli ya
mgongo.
(Badala ya kuinama, chuchumaa!!!) - Epuka kugeuka kuelekea upande upande (twisting) wakati uebeba mzigo ili kuepusha hatari ya kujeruhi misuli ya ndani katika mgongo wako.
- Kaza misuli yako ya tumbo wakati wa kubeba mizigo ili kuwianisha uhimili wa tumbo na mgongo ili kukuweka katika mkao mzuri wakati wa kubeba mzigo.
- Hakikisha unatazama mbele unaoelekea lengo likiwa ni kukuweka katika u-wima wa mgongo wako wakati wa kubeba mzigo na pia kukufanya kuwa makini ili usijikwae ukingali na mzigo.
- Anza kutembea kuelekea ulikopanga kubeba mzigo wako kuupeleka.
- Weka mzigo chini kwa kuzingatia kinyume cha mtiririko huu wa kunyenyua na kubeba mizigo (kuanzia hatua ya 8 kurudi nyuma hadi hatua ya 1) baada ya kufika na kusimama.
(Kutua mzigo ni kinyume cha hatua za kunyenyua) |
(Omba msaada) |
***Mzigo unapokuwa
mzito kuliko uwezo wako wa kuubeba, tafadhali omba/tafuta msaada ili kuondoa
hatari ya kujeruhi misuli au disk za mgongo wako***
(Mzigo ulio juu ya usawa wa mabega) |
(Fuata maelekezo/Ushauri) |
- Kama una shida ya mgongo (maumivu au jeraha)unashauriwa kuvaa mkanda wa mgongoni (back brace) kuzuia hatari ya kujeruhi/kuumiza misuli ya mgongo wako wakati wa kubeba/kunyenyua mizigo.
- Epuka kubeba/kushusha mzigo ulio juu ya usawa wa mabega yako badala yake tumia ngazi au simama juu ya meza ili uufikie vizuri.
- Pata ushauri wa kitaalmu wa namna ya kubeba uzito katika michezo au wakati wa kufanya mazoezi ili kupunguza hatari ya kujeruhi mgongo wako.
***Kwa swali au ushauri usisite kuwasiliana nami***
No comments:
Post a Comment