UTANGULIZI:
Uzito unaopita kiasi (Obesity) umekuwa ni tatizo kubwa kwa dunia
ya leo likiwa linachangiwa na mabadiliko ya hali ya maisha kwa ujumla (ikiwa ni
pamoja na mazingira). Watu wenye uzito kupita kiasi husumbuliwa na uzito wa
ziada hivyo kuwafanya kuwa na vitambi/mafuta ya ziada mwilini.
Katika hali ya sasa, uzito unaopita kiasi ni ugonjwa tena tishio
kwa vile ni chimbuko la matatizo/magonjwa mengine mengi. Watu wenye uzito wa
kupindukia wapo katika hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukiza kama vile ya
moyo (shinikizo la damu), kisukari pamoja na kiharusi (Stroke).
Kwa hali hii, uzito unopita kiasi unatambulika kama "muuaji
wa kimya kimya" kwa kuwa chanzo cha kusababisha magonjwa hatari katika
maisha ya binadamu. Pamoja na hayo yote, uzito unaozidi kiasi unaweza kuzuiliwa
au kudhibitiwa kwa njia za asili kwa kuzingatia uwiano wa urefu na uzito wa
mwili wa mtu husika (Body Mass Index - BMI).
Zilizoorodheshwa hapa chini ni njia 10 zitakazokusaidia
kupunguza uzito mwilini. Ukizifuata kwa uaminifu, utaona mabadiliko makubwa kwa
kipindi kifupi (hadi kufikia mwezi mmoja).
Kuunguza
mafuta na nishati (calories) ya ziada mwilini mwako:
- Moja ya njia nzuri zaidi ya kusaidia kuunguza mafuta na nishati ya ziada mwilini mwako ni pamoja na kufanya mazoezi kila siku kwa muda usiopungua dakika 30 (kwa maelezo zaidi juu ya aina na namna ya kufanya mazoezi haya usisite kuwasiliana nami/PHYSIOTHERAPIST aliye karibu nawe).
Lishe
bora:
- Lishe duni (ya kula chakula cha aina moja kwa wingi hasa "wanga")husababisha kongezeka uzito na matatizo ya kiafya. Vyakula vya kukaangwa kwa mafuta pekee kama vile chips, ndizi za kukaanga na vinavyofanana na hivyo (fast foods) huongeza mafuta mengi na nishati ya ziada mwilini.
- Ili kupunguza uzito, inapaswa upunguze matumizi au kuachana kabisa na kutumia vyakula vya namna hiyo.
Achana
na au punguza matumizi ya vinywaji vyenye madini ya "Carbonate":
- Vinywaji kama juisi za viwandani au soda vinakuwa na "carbonate" hivyo huwa na tabia ya kuongeza mafuta na nishati ya ziada katika mwili wako na kusababisha kuongezeka uzito mwilini.
- Mbadala wa vinywaji hivi ni kunywa juisi za matunda asilia za kutengenezwa nyumbani.
Mboga
za majani:
- Mboga za majani zinakuwa na nyuzi nyuzi muhimu katika mfumo wa umengenyaji wa chakula, lakini pia protini pamoja na vitamini muhimu hupatikana katika mboga za majani.
- Hvyo basi, badala ya kula chakula chenye wanga mwingi ni bora nafasi kubwa ikachukuliwa na mboga za majani kwa kuwa zinakuwa na nishati kiasi/kidogo na ni bora kwa afya ya mwili.
Matunda:
- Matunda si tu kwamba yana virutubisho sawa vile vinavyopatikana katika matunda lakini pia yanakuwa na "carbonate" asilia.
- Pia matunda sawa na mboga za majani, yanaimarisha kinga ya mwili na kukuepusha na magonjwa bali mbali.
Jizuie
kula bila mpangilio hasa vyakula vidogo dogo (snacks) katikati ya milo mikuu
mitatu:
- Kula vyakula kama clips za aina mabili mbali (viazi, ndizi etc), chokoleti, biskuit, pipi na vinavyofanana na hivyo ni kutafuta hatari ya kuongeza uzito wa ziada mwilni ambao ni hatari kwa afya ya mwili wako.
Punguza
matumizi ya sukari au vyakula vyenye sukari nyingi:
- Sukari inapozidi hubadilishwa na ini kisha kuhifadhiwa na mwili kama mafuta ya ziada. Kupunguza matumizi ya chakula chenye sukari nyingi husaidia katika kudumu kuwa na mwili wenye uzito sawia.
Punguza
matumizi ya chumvi:
- Chumvi inakuwa na madini mengi ya "Sodium" ambayo yana tabia ya kuongeza uzito mwilini. Upunguzaji ya vyakula hivi hupunguza maji mengi ya ziada mwilini ambayo humfanya mtu aonekana mnene!!
- (EPUKA KUONGEZEA CHUMVI (MBICHI) MEZANI!!!)
Chai
asilia (ya viungo asilia -"Green tea"):
- Chai ya viungo asilia kama vile mchai chai, tangawizi... husaidia katika kuunguza mafuta ya ziada mwilini na pia husaidi kuondoa sumu (taka mwili za sumu) mwilini.
Jaribu
kuwa asilia:
- Jiweke kuwa asilia kwa kutotumia muda mwingi katika kuangalia televisheni au kutumia au kucheza michezo ya kompyuta kwa muda mrefu kwa sababu huongeza hatari ya kuongeza uzito mwilini kwa kuwa mwili huridhika bila kufanya kazi inayowiana na chakula unachokula (kula na kulala/kukaa!!).
- Jizuie kutumia lift au usafiri kama gari, piki piki na kadhalika kwa mwendo au urefu/umbali ambao unaweza kutembea au kupanda bila shida ili kusaidia kuunguza mafuta y ziada kwa kuufanyisha mwli kazi.
(Kwa swali/ushauri wa namna ya kupunguza mafuta mwilini (na
mazoezi kwa ujumla), usisite kuwasilina nami)
Thanks John for such an educative blog.
ReplyDelete