Search This Blog

Monday, 22 August 2016

MAZOEZI NI NINI?

SEHEMU A: UTANGULIZI

Nini maana ya mazoezi?
Mazoezi ni shughuli inayopangiliwa kufanyika katika muundo na muda fulani kwa malengo mahususi ya kuimarisha mwili.

Mpangilio (plan):
Kujiweka tayari kwa ajili ya mazoezi katika siku/muda fulani.

Muundo (structure):
Namna ya kufanya na aina ya mazoezi ya kufanya katika siku au muda husika.

Muda (time):
Muda maalumu wa kufanya mazoezi kwa siku/wiki na wa kujirudia rudia (mara ngapi kwa siku/wiki).

Lengo la mazoezi (objective/aim):
Kuimarisha mwili katika nyanja mojawapo ikiwemo nguvu, pumzi, kulainisha viuongo, kunyoosha misuli, n.k.

SEHEMU B: AINA ZA MAZOEZI

Mazoezi yamegawanyika katika makundi makuu manne:
1.       Mazoezi ya kuongeza pumzi (aerobic (endurance training) exercises)
Mfano: kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli, michezo ya aina mbali mbali.

2.       Mazoezi ya kuongeza nguvu (strengthening exercises)
Mfano: kunyenyua/kubeba uzito wa aina mbali mbali.

3.       Mazoezi ya kulainisha viungo (flexibility exercises)
Mfano: kurefusha misuli na kulainisha viungo.

4.       Mazoezi ya kuongeza stamina (balance/stability training exercises)
Mfano: kusimama kwa mguu mmoja kwa sekunde/dakika kadhaa, n.k.

SEHEMU C: MFANO: KUKIMBIA

Mpangilio  =   Unapanga kufanya mazoezi asubuhi/jioni
Muundo     =   Kukimbia umbali fulani
Muda         =   Nusu saa kwa siku
Marudio     =   Mara tatu kwa wiki (Jumapili, Jumanne na Ijumaa)
Lengo        =   Kuimarisha pumzi

SEHEMU D: FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI

Mazoezi yananufaisha mwili kwa namna mbali mbali. Miongoni mwa faida za mazoezi katika mwili ni pamoja na:
1.       Kupunguza na kudhibiti uzito na mafuta mwilini (controls weight)
2.       Kudhibiti kiwango cha lehemu mwilini (controls cholesterol)
3.       Kuongeza uwezo wa mwili kuhimili vishindo (mf. Kuteguka, kuvunjika)  kwa kuimarisha misuli na mifupa
4.       Kuimarisha uwezo wa moyo katika kusukuma damu (strengthening of heart muscles)
5.       Kuongeza uwezo wa kufanya kazi (physical fitness)
6.       Kuongeza uwezo wa mwili wa kuzalisha na kutumia nishati
7.       Kudhibiti kiwango cha sukari katika mzunguko wa damu mwilini (stabilizes blood sugar levels)
8.       Kuimarisha mzunguko wa damu (improves microcirculation)
9.       Kuimarisha usingizi (improves sleep)
10.   Kubadili na kupendezesha mwonekano wa mwili (body appearance/shape)
11.   Kuimarisha na kulainisha viungo pamoja na misuli (increase flexibility)
12.   Kupunguza na kuzuia msongo wa mawazo (minimizes the chances of depression)
13.   Kuimarisha stamina (stability, balance and coordination)
14.   Kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya tabia kama vile: magonjwa ya moyo, kisukari, n.k (sedentary lifestyle diseases)
15.   Kuimarisha mahusiano ya ndoa (sexual realationship)**

**Kitaalam, mazoezi yanasadikika kuongeza uzalishaji wa vichocheo vya mwili vinavyohusika na ama kuwa na hamu au kuongeza uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
**Vile vile mazoezi huwaweka wapendanao karibu zaidi hasa pale wanapokuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya pamoja.

SEHEMU E: CHA KUZINGATIA:
Muundo: (Frequency (F), Intensity (I), Type (T), Time (T) [FITT PRINCIPLE])
  • Mara ngapi unafanya mazoezi kwa siku/wiki
  • Kiasi au ugumu wa mazoezi/shughuli husika
  • Muda kiasi gani wakati wa kufanya mazoezi
  • Aina ya mazoezi/shughuli


Kwa msaada zaidi wa kujua kuhusu aina sahihi ya zoezi linalofaa kwa tatizo husika, kama vile, kisukari, magonjwa ya moyo, n.k. bofya hapa




No comments:

Post a Comment