SEHEMU A: UTANGULIZI
Nini maana ya mazoezi?
Mazoezi ni shughuli inayopangiliwa
kufanyika katika muundo na muda fulani kwa malengo mahususi ya kuimarisha
mwili.
Mpangilio (plan):
Kujiweka tayari kwa ajili ya mazoezi
katika siku/muda fulani.
Muundo (structure):
Namna ya kufanya na aina ya mazoezi ya
kufanya katika siku au muda husika.
Muda (time):
Muda maalumu wa kufanya mazoezi kwa
siku/wiki na wa kujirudia rudia (mara ngapi kwa siku/wiki).
Lengo la mazoezi (objective/aim):
Kuimarisha mwili katika nyanja mojawapo
ikiwemo nguvu, pumzi, kulainisha viuongo, kunyoosha misuli, n.k.
SEHEMU B: AINA ZA MAZOEZI
Mazoezi yamegawanyika katika makundi makuu
manne:
1.
Mazoezi ya kuongeza pumzi (aerobic (endurance training) exercises)
Mfano:
kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli, michezo ya aina mbali mbali.
2.
Mazoezi ya kuongeza nguvu (strengthening exercises)
Mfano:
kunyenyua/kubeba uzito wa aina mbali mbali.
3.
Mazoezi ya kulainisha viungo (flexibility exercises)
Mfano:
kurefusha misuli na kulainisha viungo.
4.
Mazoezi ya kuongeza stamina (balance/stability training exercises)
Mfano:
kusimama kwa mguu mmoja kwa sekunde/dakika kadhaa, n.k.
SEHEMU C: MFANO: KUKIMBIA
Mpangilio = Unapanga
kufanya mazoezi asubuhi/jioni
Muundo = Kukimbia umbali fulani
Muda =
Nusu saa kwa siku
Marudio = Mara
tatu kwa wiki (Jumapili, Jumanne na Ijumaa)
Lengo = Kuimarisha pumzi
SEHEMU D: FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI
Mazoezi yananufaisha mwili kwa namna
mbali mbali. Miongoni mwa faida za mazoezi katika mwili ni pamoja na:
1. Kupunguza na kudhibiti uzito na mafuta mwilini (controls weight)
2. Kudhibiti kiwango cha lehemu mwilini (controls cholesterol)
3. Kuongeza uwezo wa mwili kuhimili vishindo (mf. Kuteguka,
kuvunjika) kwa kuimarisha misuli na
mifupa
4. Kuimarisha uwezo wa moyo katika kusukuma damu (strengthening of heart muscles)
5. Kuongeza uwezo wa kufanya kazi (physical fitness)
6. Kuongeza uwezo wa mwili wa kuzalisha na kutumia nishati
7. Kudhibiti kiwango cha sukari katika mzunguko wa damu mwilini
(stabilizes blood sugar levels)
8. Kuimarisha mzunguko wa damu (improves microcirculation)
9. Kuimarisha usingizi (improves
sleep)
10. Kubadili na kupendezesha mwonekano wa mwili (body appearance/shape)
11. Kuimarisha na kulainisha viungo pamoja na misuli (increase flexibility)
12. Kupunguza na kuzuia msongo wa mawazo (minimizes the chances of depression)
13. Kuimarisha stamina (stability,
balance and coordination)
14. Kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya tabia kama vile: magonjwa
ya moyo, kisukari, n.k (sedentary lifestyle
diseases)
15. Kuimarisha mahusiano ya ndoa (sexual realationship)**
**Kitaalam, mazoezi yanasadikika kuongeza uzalishaji wa vichocheo vya mwili vinavyohusika na ama kuwa na hamu au kuongeza uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
**Vile vile mazoezi huwaweka wapendanao karibu zaidi hasa pale wanapokuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya pamoja.
SEHEMU E: CHA KUZINGATIA:
Muundo: (Frequency (F), Intensity (I), Type (T), Time (T)
[FITT PRINCIPLE])
- Mara ngapi unafanya mazoezi kwa siku/wiki
- Kiasi au ugumu wa mazoezi/shughuli husika
- Muda kiasi gani wakati wa kufanya mazoezi
- Aina ya mazoezi/shughuli
Kwa msaada zaidi wa kujua kuhusu aina sahihi ya
zoezi linalofaa kwa tatizo husika, kama vile, kisukari, magonjwa ya moyo, n.k.
bofya hapa